TANZANIA-SIASA-UCHAGUZI-DAR ES SALAAM-CHADEMA-CCM

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu auawa katika maandamano ya upinzani Tanzania

Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT aliyefariki dunia jana bada ya kupigwa risasi na polisi Mjini Dar es Salaam
Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT aliyefariki dunia jana bada ya kupigwa risasi na polisi Mjini Dar es Salaam facebook

Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) nchini Tanzania, Akwiilina B Akwilina ameuawa wakati jeshi la polisi lilipotumia mabomu ya machozi na risasi kuwatawanya wafuasi wa chama kikuu cha upinzani cha Chadema.

Matangazo ya kibiashara

Tukio hili limetokea jana wakati wafuasi wa Chadema na viongozi wao walipoandamana kwenda kwa msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni kudai fomu za mawakala wao. Wafuasi kadhaa wa Chadema wanashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Profesa Prof. Zacharia Mganilwa wakati akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya BBC ameeleza kuwa mwanafunzi wao wa shahada ya Manunuzi na Ugavi Akwilina Akwilini alifariki dunia siku ya Ijumaa.Amesema mwili wa msichana huyo umekutwa na jeraha la risasi kichwani.

Kwa mujibu wa uongozi huo wa chuo hicho, mwanafunzi huyo alikuwa akielekea Bagamoyo kupeleka fomu za kuomba nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo mjini Bagamoyo mkoani Pwani.

Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amekiri kuwa mtu mmoja alipigwa risasi na kuuawa wakati polisi walipokuwa wakitawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakiandamana.

Uchaguzi katika majombo ya Kinondoni Mkoani Dar es Salaam na Siha Mkoani Kilimanjaro unafanyika baada ya waliokuwa wabunge wa majombo hayo, Maulid Mtulia na Dr Godwin Mollel kujiuzulu nyadhifa zao.