RWANDA-UFARANSA

Waziri wa Michezo wa Ufaransa amalizia ziara yake nchini Rwanda

Waziri wa Midhezi wa Ufaransa Laura Flessel
Waziri wa Midhezi wa Ufaransa Laura Flessel www.rfi.fr

Waziri wa Michezo wa Ufaransa Laura Flessel, anamaliza ziara yake nchini Rwanda baada ya kuwasili nchini humo siku ya Alhamisi kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kimichezo kati ya nchi hizo mbili.

Matangazo ya kibiashara

Katika ziara hiyo, Waziri Flessel, alikutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Julienne Uwacu, jijini Kigali.

Waziri Flessel amesema kupitia michezo mataifa hayo mawili yanaweza kuimarisha uhusiano wao kwa lengo la kusaidiana  kuinua hali ya elimu, afya, uchumi na mambo mengine kati ya nchi hizo mbili.

Waziri huo ametembelea shule lugha ya Kifaransa Antoine-de-Saint-Exupéry jijini Kigali na kukutana na wanafunzi na kuhimiza umuhimu wa kutumia michezo kuimarisha lugha.

Hii ni ziara ya kwanza ambayo imefanywa na waziri anayehudumu katika serikali ya rais Emmanuel Macron. Rais wa zamani Nicolas Sarkozy mapema mwaka huu pia alizuru Rwanda.

Wadadisi wa siasa wanaona kuwa ziara kama hizi, ni mbinu za kidiplomasia kujaribu kurejesha uhusiano wa zamani kati ya mataifa haya mawili.

“Uhusiano baina ya Rwanda na Ufaransa si mbaya kwa sababu tuna mabalozi kutoka nchi hizi mbili na Wanyarwanda wanaendelea kwenda Ufaransa na wao wanakuja kuja, nafahamu mambo si mazuri sana lakini si mabaya, “ alisema Waziri wa Rwanda Uwacu Julienne .

Uhusiano wa Ufaransa na Rwanda ulianza kuyumba baada ya Ufaransa walipotoa hati ya kuwakamata maofisa wa juu wa jeshi la Rwanda RDF kwa madai kuwa walihusika katika utunguaji wa ndege ya aliyekuwa rais wa Rwanda wakati huo Juvenal Habyarimana na kuzua mauaji ya kimbari mwaka 1994.