MAREKANI-RWANDA-TANZANIA-UGANDA-UCHUMI

Marekani kuchukua vikwazo dhidi ya nchi zinazopiga marufuku mitumba

Wafanyabiashara katika soko la nguo na viatu vilivyotumika, Kigali, Rwanda, Juni 30, 2016.
Wafanyabiashara katika soko la nguo na viatu vilivyotumika, Kigali, Rwanda, Juni 30, 2016. RFI/Stéphanie Aglietti

Tangu mwaka 2016, nchi tatu za Afrika Mashariki Afrika, ikiwa ni pamoja na Uganda, Tanzania na Rwanda ziliamua kupiga marufuku uagizaji wa nguo na viatu vilivyotumika (Mitumba) kutoka Ulaya au Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Lengo la sheria hii, ambayo itaanza kutumika mwaka 2019, ni kuinua viwanda vya nguo na ngozi katika kanda ya Afrika Mashariki.

Uamuzi huu wa Tanzania, Uganda na Rwanda unakabiliwa na upinzani kutoka Marekani na hasa kampuni ya Materials and Recycled Textils Association (SMART).

Marekani inaagiza kila mwaka nguo zilizotumika zenye thamani ya dola milioni 124 kwa nchi hizi tatu.

Pia, uamuzi huu unaonekana kuwa ni ukiukwaji wa sheria za kuhusu mkataba wa kibiasha wa AGOA (African Growth Opportunity Act)) ambao unaondoa vikwazo vya biashara na Marekani.

Sehemu kubwa ya bidhaa hizi zinazoagizwa katika chi hizi tatu ni nguo zilizotumika (Mitumba).

Lakini Belinda Edmonds, Mkurugenzi Mtendaji wa African Cotton and Textile Industries (ACTI), chama kinachojumuisha wanachama wa viwanda vya pamba na nguo kutoka nchi 24 za Afrika, anaamini kuwa kuwekwa kwa vikwazo hivi hakukiuki sheria ya AGOA, hasa kwa ibara yake ya 3703 (1) (C) kuhusu kuondoa vikwazo vya biashara na uwekezaji na Marekani.

"Sehemu kubwa ya nguo zinazoagizwa katika nchi za Uganda, Tanzania na Rwanda hazitengenezwi nchini Marekani, " amesma Belinda Edmonds.

Chini ya shinikizo la Marekani, Kenya, ambayo lilikuwa imeshirikiana na majirani zake kwa marufuku hayo dhidi ya Mitumba imeamua kujiondoa kufuatia tishio la kupoteza unafasi kwenye soko la Marekani ambayo ni mshirika wake wa tatu wa kibiashara. Rwanda, Uganda na Tanzania wamesisitiza nia yao ya kuendelea na marufuku hiyo. Ikumbukwe kwamba kwa nchi hizi, mauzo ya nje kwa Marekani yalifikia dola milioni 43 tu mwaka 2016 ikilinganishwa na dola milioni 281 katika uagizaji mwaka huo. Kwa mujibu wataala wa masuala ya uchumi , Afrika Mashariki inauza nguo zilizotumika kutoka Marekani na Ulaya zenye thamani ya dola milioni 350 na kiwango hiki ni sawa na asilimia 60 kila mwaka.

Wakati huo huo, pamba ni bidhaa ya tatu inayoingizia fedha za kutosha nchi ya Uganda ikifuatiwa na kahawa na chai, na hunufaisha familia 250,000.

"Hata kama tunajaribu kuelewa hoja ya nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu uagizaji wa nguo na viatu vilivyotumika kama moja ya sababu zinazofanya viwanda vya nguo na ngozi kusambaratika na hivyo kuwanyima wenyeji nafasi ya ajira, tunaamini kwamba marufuku haya hayatochangia kwa kuinua viwanda hivyo. Mpaka sasa tunajiuliza kama kweli raia kutoka nchi hizi watakua na uwezo wa kununua bidhaa hiyo (nguo) kwenye soko la EAC, "amesema Harry Sullivan, ambaye anahusika na masuala ya kiuchumi ya Afrika katika wizara ya mashauriano ya kigeni ya Marekani.