BURUNDI-OCHA-MSAADA-USALAMA

Burundi yapinga ripoti ya OCHA kuhusu raia wake wanaohitaji msaada wa kibinadamu

Wakimbizi hao wa Burundiwalitoroka makazi yao na kukimbilia nchini Tanzania wakipitia pwani ya Ziwa Tanganyika huko Kagunga, kaskazini mwa Tanzania.
Wakimbizi hao wa Burundiwalitoroka makazi yao na kukimbilia nchini Tanzania wakipitia pwani ya Ziwa Tanganyika huko Kagunga, kaskazini mwa Tanzania. REUTERS/Thomas Mukoya

Serikali ya Burundi imefutilia mbali ripoti ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kibinadamu, OCHA, ambayo inasema kuwa watu milioni 3.6 wa Burundi wanahitaji msaada.

Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Burundi inasema ripoti hiyo ilitolewa na upande umoja bila kushirikishwa na inaiomba OCHA kuwasiliana na wizara nne husika kwa minajili ya kutoa ripoti nyingine "ambayo watakua "wamekubaliana na ya kuaminika" ili kuwasaidia wale wanaohitaji msaada wa kibinadamu mwaka 2018.

Hata hivyo, siku ya Jumatatu wakati ripoti ya Umoja wa Mataifa ilitolewa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje alikuepo.

Taarifa ya katibu mkuu na msemaji wa serikali, Philippe Nzobonariba, inafutilia mbali yaliyomo katika ripoti ya OCHA ambayo inasema kuwa watu milioni 3.6 wa Burundi wanahitaji msaada wa kibinadamu.

>> Soma pia: UN yahitaji dola Milioni 270 kusaidia wakimbizi kutoka Burundi na DRC

Kwa mujibu wa ripoti ya Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu, watu milioni 2.4 nchini Burundi wanakabiliwa na hali ya dharura ya kibinadamu mwaka huu na watahitaji msaada wa kibinadamu kutoka Umoja wa Mataifa wa dola milioni 141.7.

Serikali ya Burundi inathamini mpango wa jumuiya ya kimataifa kusaidia watu wanaokabiliwa na hali ya dharura. laikini imefutilia mbali ripoti hiyo ya OCHA ikisema kuwa, ripoti hiyo inaoyesha hali ya kutisha mbali na ukweli.

Serikali ya Burundi inatarajia washirika wake kutoa zaidi misaada ya maendeleo kuliko kutoa misaada ya kibinadamu.