EAC-MIRADI-UCHUMI

EAC inahitaji Dola Bilioni 78 kufanikisha miradi ya miundombinu

Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakikutana jijini Kampala nchini Uganda Februari 22 2018
Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakikutana jijini Kampala nchini Uganda Februari 22 2018 /www.eac.int

Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inahitaji Dola za Marekani Bilioni 78 kufanikisha miradi mbalimbali ya miundo mbinu kwa lengo la kuimarisha uchumi katika Jumuiya hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa Jumuiya hiyo wakikutana jijini Kampala, wamekubaliana kuwa Dola Bilioni 62 zitatengewa ujenzi wa reli ya kati, barabara na mradi wa nguvu za umeme.

Kilomita 7,600 za barabara, reli ya kali Kilomita 4,000 na Megawats 6734 zinatarajiwa kujengwa katika mataifa yote sita ya Jumuiya hiyo.

Kukamilika kwa miradi hii, itasaidia pia kurahihisha usafiri wa watu na bidhaa pamoja na kuinua uzalishaji wa bidhaa.

Miradi ya afya pia inatarajiwa kuimarishwa ikiwa ni pamoja na kujenga taasisi za afya, utafiti na dawa kwa lengo la kuwasaidia wakaazi wa nchi za Afrika Mashariki.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa kati ya Dola Bilioni 78 za Marekani, ni Dola Bilioni 5 ndizo zilizopatikana kuanza kwa miradi hii. Jumuiya hiyo inatarajia ufadhili kutoka Mataifa ya Ulaya kufanikisha miradi hiyo.

Miradi hii inatarajiwa kumalizika kufikia mwaka 2025.