BURUNDI

Vijana wa chama tawala Burundi waandamana usiku

Kulingana na ripoti ya HRW , vijana wa chama tawala cha Cndd-Fdd Imbonerakure,  walishiriki katika mauaji ya kikatili mkoani Cibitoke kati ya Desemba 30 na Januari 3.
Kulingana na ripoti ya HRW , vijana wa chama tawala cha Cndd-Fdd Imbonerakure, walishiriki katika mauaji ya kikatili mkoani Cibitoke kati ya Desemba 30 na Januari 3. Desire Nimubona/IRIN/www.irinnews.org

Zaidi ya vijana elfu mbili kutoka chama tawala nchini Burundi maarufu kama Imbonerakure wamefanya maandamano jimboni Muyinga kaskazini mashariki mwa nchi usiku wa ijumaa kuamkia jumamosi,kwa mujibu wa mashuhuda.

Matangazo ya kibiashara

Wakieleza kwa masharti ya kutotajwa majina yao baadhi ya wakazi wa eneo hilo wameiambia Afp Kwamba walishtushwa na sauti za nyimbo miluzi na michezo kadhaa ya vijana wa imbonerakure waliokusanyika kuanzia saa nane za usiku.

 

Vijana wa rika mbalimbali waliendelea kukusanyika hadi saa kumi na mbili asubuhi kabla ya kujikusanya katika uwanja wa mpira wa miguu na kutoleana hotuba mbalimbali.

Kundi la vijana wa chama cha CNDD FDD Imbonerakure wamekuwa wakitajwa kuingilia usalama wa nchi hiyo kwa kudhibiti na kuzuia uvukaji wa mipaka kuingia nchi jirani za Rwanda na Tanzania hasa kwa warundi wanaojaribu kusaka hifadhi huko.

Vilevile wamekuwa wakijiihusisha na doria za usiku na kuanzisha vituo kadhaa vya ukaguzi wa barabarani AFP inaarifu.