Pata taarifa kuu
RWANDA-KENYA-BURUNDI-TABIA NCHI

Mvua zinazonyesha zaua watu 18 Rwanda

Wanawake hawa wakifanya shughuli yao ya kilimo magharibi mwa Rwanda, Lakini wakulima wengi wamesema mvua zimeharibu mashamba yao.
Wanawake hawa wakifanya shughuli yao ya kilimo magharibi mwa Rwanda, Lakini wakulima wengi wamesema mvua zimeharibu mashamba yao. RFI/Stéphanie Aglietti
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Mvua kubwa imeendelea kunyesha katika mataufa ya Afrika Mashariki na Kati. Nchini Rwanda watu kumi na wanane wamepoteza maisha wiki hii, baada ya kusumbwa na maji.

Matangazo ya kibiashara

Mbali na maaafa hayo, makaazi ya watu yameharibika hasa wale wanaoishi katika maeneo ya milima.

Nchini Kenya, hali imekuwa vivyo hivyo baada ya mvua kubwa inayoendelea kunyesha kusababisha madhara makubwa, ikiwa ni pamoja na baadhi ya mitaa ya jiji kuu Nairobi kama Buruburu kujaa maji.

Nchini Burundi, hasa katika mji mkuu wa nchi hiyo Bujumbura, maeneo ya Maramvya, Carama na maeneo ya mabondeni ndio yameathrika zaidi na mvua hizo zinazoendelea kunyesha.

Wakulima kwa upande wao wanasema kuwa hawaamini kuwa msimu huu watapata mavuno ya kutosha.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.