Pata taarifa kuu
TANZANIA-UFARANSA-UTAMADUNI

RFI Kiswahili na Alliance Francaise waadhimisha siku ya Muziki wa Jazz

Album «Radio One» d'Airelle Besson
Album «Radio One» d'Airelle Besson

Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa Alliance Francais kwa kushirikiana na Idhaa ya kiswahili ya Rfi inaungana na shirika la umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO kuadhimisha siku ya kimataifa ya muziki wa jazz wakati ambapo idhaa hiyo inaelekea kuadhimisha miaka minane ikitangaza kwa lugha ya kiswahili.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumzia sherehe hizo za Siku ya Jazz Mkurugenzi wa Alliance Francais jijini Dar es salaam.Frederic Tiberti amesema Wasanii watakao tumbuiza ni Airelle Besson akiwa ni miongoni mwa wanamuziki wawili wa muziki wa jazz kutoka nchini Ufaransa.

“Ni miongoni mwa wasanii maarufu sana nchini Ufaransa wanaofanya muziki huu na jina lake ni Lionel Suarez na wa pili ni Airelle Besson ni Mwanamuziki mwingine anayekuja kwenye tamasha hili na ni mwanamke anayepiga kifaa cha ara ya upepo “ alisema Frederic Tibert.

Akizungumzia umuhimu wa Usiku wa jazz, Mkuu wa Idhaa ya kiswahili ya rfi, Robert Minangoy amesema lengo ni kuimarisha mtengamano baina ya wafaransa na jamii nyingine licha ya utofauti wa tamaduni wakati huu ambapo Idhaa hii ikielekea kutimiza miaka minane.

“ Ni Fursa nzuri kubadilishana utamaduni wa wafaransa ,pamoja na kusherehekea maadhimisho yetu ,najua mnaifahamu rfi kiswahili tunasikika nchini Tanzania na pia katika nchi za ukanda wa Afrika mashariki “ alisema Minangoy.

Idhaa hii inatimiza miaka minane hapo July 05 mwaka huu ikiwafikia wazungumzaji wa lugha ya kiswahili Duniani kote.

Ripoti ya Mwandishi wa Rfi Kiswahili, Steven Mumbi.

 

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.