KENYA-TABIA NCHI

Maelfu ya watu waokolewa kwa ndege za kijeshi Kenya

Maeneo kadhaa yamekumbwa na mafuriko nchini Kenya kufuatia mvua inayoendelea kunyesha.
Maeneo kadhaa yamekumbwa na mafuriko nchini Kenya kufuatia mvua inayoendelea kunyesha. AFP/Brenda Bannon

Mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi ya Kenya na kusababisha mafuriko makubwa, imesababisha serikali ya nchi hiyo kutumia ndege za kijeshi kuwaokoa watu 18,000 katika Kaunti ya Kilifi Pwani ya nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Shirika la Msalaba mwekundi linasema, maelfu ya watu wanahitaji msaada wa haraka baada ya makaazi yao kusombwa na maji katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Hali ni mbaya katika Kaunti ya Kilifi, baada ya maji kuvunja kingo za mto Sabaki na kusababisha maji kuingia ndani ya makaazi ya watu.

Hivyo ndivyo hali ilivyo katika kambi kubwa ya wakimbizi inayowapa hifadhi raia wa Somalia waliokimbilia nchini humo.

Watoto wapo hatarini kupata magonjwa kama vipindupindu kutokana na maji kujaa karibu na hema zinazowapa hifadhi.

Viwanja vya michezo pia vimejaa maji katika kambi hiyo, huku watoto wakionekana wakikimbizana majini na kucheza, katika mazingira hatari.

Maeneo mengine ambayo yameathiriwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha ni pamoja na Kaunti ya Garisa, eneo ambalo pia makaazi ya watu yamejaa maji.

Watalaam wa utabiri wa hali ya hewa nchini humo wanaonya kuwa mvua kubwa itaendelea kunyesha nchini humo.