MAREKANI-KENYA-SUDAN-KUSINI-VIKWAZO-SIASA

Marekani yaitaka Kenya kuchunguza mali za viongozi Sudan Kusini

Kiongozi wa waasi, Riek Machar (kulia) na rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir (kushoto) Mei 9 mwaka 2014.
Kiongozi wa waasi, Riek Machar (kulia) na rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir (kushoto) Mei 9 mwaka 2014. REUTERS/Goran Tomasevic

Nchi ya Marekani inaitaka Serikali ya Kenya kuchunguza mali zinazomilikiwa na familia za wasomi kutoka Sudan Kusini, zikiwemo mali za aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar na rais Salva Kiir, mali ambazo Marekani inasema viongozi hao wamewekeza nchini Kenya.

Matangazo ya kibiashara

Katibu mkuu wa wizara ya fedha wa Marekani aliyeko chini ya mkuu wa kitengo cha kupambana na ugaidi Sigal Mandelker akitembelea nchi ya Kenya, amesema baadhi yao wako kwenye orodha ya vikwazo na wameendelea kutakatisha fedha wakiitumia nchi hiyo.

Mandelker anasema ikiwa Kenya itashindwa kuchunguza tuhuma hizi na kuchukua hatua, Marekani haitasita kuiwekewa vikwazo.

Marekani inasema inao ushahidi wa kutosha kuonesha namna familia na viongozi wa Sudan Kusini wamekuwa wakiwekeza nchini Kenya kwa kutumia fedha za uma huku wengi wakiwa kwenye orodha ya watu waliowekewa vikwazo.