SUDANI KUSINI-SIASA-USALAMA

Rais wa Sudani Kusini na mpinzani wake wakutana Khartoum

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na mpinzani wake Riek Machar wakiwa pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni na Rais wa Sudan Omar al-Bashir huko Khartoum tarehe 25 Juni 2018.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na mpinzani wake Riek Machar wakiwa pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni na Rais wa Sudan Omar al-Bashir huko Khartoum tarehe 25 Juni 2018. © AFP

Rais wa Sudani Kusini Salva Kiir na mpinzani wake Riek Machar wamekutana mjini Khartoum, nchini Sudani, Jumatatu wiki hii kufufua mchakato wa amani uliokwama katika nchi hiyo changa barani Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Sudani Kusini inaendelea kukumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 2013.

Mazungumzo hayo, ambayo yanafuata mkutano wa kikanda wa mataifa ya Afrika Mashariki (IGAD) nchini Ethiopia ili kufufua mchakato wa amani nchini Sudani Kusini, yamefanyika wakati ambapo hivi karibuni Umoja wa Mataifa ulitoa muda hadi mwishoni mwa mwezi Juni kwa makundi hasimu kuwa yamefikia " mkataba wa kisiasa unaofaa ", huku ukitishia kuwachukulia vikwazo.

Jumatatu wiki hii, wawili hawa wamekutana katika jumba la mikutano mjini Khartoum mbele ya Marais wa Sudan Omar al-Bashir na Yoweri Museveni wa Uganda, lkwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

Salva Kiir na Riek Machar walipeana mikono mbele ya Rais Bashir na Museveni.

Sudan Kusini ilipata uhuru kutoka Sudan mnamo mwaka 2011. Nchi hii ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwishoni mwa mwaka 2013 wakati Kiir alimshtumu makamu wake wa zamani, Riek Machar kupanga mapinduzi.

Kwa raundi hii ya mazungumzo, ambayo ni ya kwanzakufanyika Khartoum kati ya viongozi hawa wawili wa Sudan Kusini tangu 2013, Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Al-Dirdiri Mohamed Ahmed ameelezea mbele ya vyombo vya habari matumaini yake ya kufikia "mkataba wa kudumu."

Mwanzoni mwa mwezi Juni, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilisitishia viongozi wa makundi yanayokinzana Sudan Kusini kuwawekea vikwazo ikiwa watashindwa kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe.