TANZANIA-MAWASILIANO

Jamii Forums warudi hewani

Nembo ya mtandao wa Jamii Forum ambao umefungwa Tanzania
Nembo ya mtandao wa Jamii Forum ambao umefungwa Tanzania Screenshot/Youtube

Jukwaa mashuhuri nchini Tanzania, Jamii Forums limeonekana kurejea hewani baada ya kutoonekena kwa wiki mbili. Lilitoweka hewani Juni 10 kufuatia kuanza kutekelezwa kwa kanuni ya mtandao zilizotungwa chini ya sheria ya Mawasiliano ya kielektroniki na posta.

Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi wa mtandao huo, Maxence Mello alithibitishia RFI kurejea hewnai kwa mtandao huo na kueleza kuwa watumiaji hawataweza kupakia maudhumi mapya badala yake wataendelea kusoma maudhui ya zamani.

Aliongeza kuwa hatua za kurejesha oparesheni zote kama ilivyokuwa awali zinaendelea kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Kaimu Meneja wa Mawasiliano wa TCRA, Semu Mwakyanjala mapema wiki hii aliambia RFI, kuwa mamlaka hiyo imeongeza muda kwa tovuti na blogs ambazo hazikujisali hadi Juni 30 mwaka huu.