SUDANI KUSINI-UGANDA

Rieck Machar kurejelea umakamo wa raisi Sudani Kusini baada ya makubaliano

Kiongozi wa waasi nchini Sudani kusini Dokta Rieck Machar
Kiongozi wa waasi nchini Sudani kusini Dokta Rieck Machar ASHRAF SHAZLY / AFP

Kiongozi wa waasi nchini Sudani kusini Dokta Rieck Machar ameridhia kurejea katika wadhifa wake wa awali wa makamo wa raisi nchini Sudan Kusini baada ya makubaliano ya mgawanyo wa madaraka kufikiwa kati yake na raisi wa taifa hilo Salva Kiir.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Al-Dierdiry Ahmed amethibitisha kuwa pande zote zimekubali kuwa na makamo wanne wa raisi,wawili waliopo sasa lakini pia Rieck Machar kurejea katika nafsi hiyo na nafasi ya nne itajazwa na mwanamke atakayechaguliwa kutoka upande wa upinzani.

Hatua hiyo imefikiwa katika majadiliano ya siri yaliyofanyika mjini Kampala nchini Uganda.

Makubaliano ya sasa ni sehemu ya jitihada za jumuiya ya kikanda kufufua mazungumzo ya amani yaliyolenga kumaliza mzozo uliogharimu maisha ya maelfu ya raia na mamilioni kukimbia makazi yao tangu Decemba 2013.

Vita ilianza baada ya raisi Kiir kumtuhumu aliyekuwa makamo wake Machar,kuwa aliandaa njama za kumpindua.