TANZANIA-SIASA-USALAMA-HAKI

Wanasiasa zaidi ya 20 wa upinzani waachiliwa kwa dhamana Tanzania

Wafuasi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, wakiwa kwenye moja ya mikutano ya chama hicho wakati wa kampeni za urais mwaka jana.
Wafuasi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, wakiwa kwenye moja ya mikutano ya chama hicho wakati wa kampeni za urais mwaka jana. RFI

Wanasiasa zaidi ya 20 wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na mbunge mmoja, ambao walikamatwa Jumamosi juma lililopita kusini mwa nchi hiyo, waliachiliwa kwa dhamana Jumatatu wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

"Watu waliokamatwa siku ya Jumamosi wameachiliwa kwa dhamana" Jumatatu asubuhi, Mkuu wa polisi katika eneo hilo, Mathias Nyange, ameliambia shirika la habari la AFP, hata kama alisema alikua hana taarifa yoyote juu ya mashtaka dhidi yao.

Kwa mujibu wa chama chake, Chadema, Mbunge Frank Mwakajoka, aliyechaguliwa katika eneo la Tunduma, alikamatwa siku ya Jumamosi katika ofisi ya wilaya yake ambapo alikwenda kuomba fomu kwa wagombea wa chama chake katika uchaguzi wa manispaa uliopangwa kufanyika Agosti mwaka huu.

Wakati huo huo polisiiliwakamata "wanachama wengine ishirini wa Chadema, ambao walikua walikusanyika katika makao makuu ya chama wilayani hapo," chanzo hicho kilisema.

"Nimepata taarifa kwamba wotewaliachiliwa kwa dhamana asubuhi hii (Jumatatu)," amethibitisha Vincent Mashinji, katibu mkuu wa Chadema.

Kwa mujibu wa Bw Mashinji, mbunge Mwakajoka anashutumiwa "kuchochea vurugu" na wengine wanashutumiwa "kuuchoma moto nyumba ya mgombea" wa chama tawala, CCM, katika uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa wa Agosti 12.

Chama cha Chadema mara nyingi kinashtumu polisi kwamba imekua ikipanga tuhuma zisizokua na msingi dhidi ya wanachama wake, kwa lengo la kudhoofisha chama, madai ambayo Wizara ya Mambo ya Ndani imekanusha.

Mnamo mwezi Septemba 2017, Mbunge wa Chadema Tundu Lissu, alijeruhiwa kwa baada ya kupigwa risasi nyingi nyumbani kwake. Mnamo mwezi Februari, viongozi wawili wa Chadema waliuawa na watu wasiojulikana.