Pata taarifa kuu
RWANDA-USALAMA

Kundi jipya la waasi la MRDC latangaza vita dhidi ya utawala wa Kagame Rwanda

Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Rais wa Rwanda Paul Kagame. REUTERS/Jean Bizimana
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Siku mbili baada ya kundi jipya la waasi la MRDC kutangaza vita dhidi ya utawala wa rais wa Rwanda Paul, Kagame, serikali ya nchi hiyo imesema kuwa madai ya mtu anayedai kuwa msemaji huyo Callixte Sankara Nsabimana ni ya uongo.

Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni Callixte meja Callixte Sankara Nsabimana anayedai kuwa msemaji wa kundi hilo, alisem akuwa lengo la vita hivyo ni kuung'oa utawala wa Kagame na kubaini kwamba ni mwezi mzima sasa tangu majeshi ya kundi lake yakipigana na majeshi ya Rwanda katika msitu wa Nyungwe kusini mwa nchi hiyo.

Ameongeza kwamba majeshi yao yaliendesha mashambulizi ymnamo mwezi Juni katika kijiji cha Nyabimata karibu na msitu wa Nyungwe.

Kwa upande wake inspekta mkuu wa polisi Emmanuel Gasana amefutilia mbali madai ya kuepo kwa kundi la waasi katika msitu wa Nyungwe, huku akihakikisha kwamba kuna majambazi wachache ambao wamekua wakivuka na kuingia Rwanda na kuwapora watu katika kijiji cha Nyaruguru. Lakini polisi ilishughulikia vilivyo hali hiyo na majambazi hao waliweza kukimbilia eneo walitoka.

Meja Callixte Sankara Nsabimana, anatoka kabila la Tutsi na ni mjombake kiongozi wa upinzani aliye kizuizini nchini Rwanda Diane Rwigara. Meja Callixte Sankara amesema ni mwanajeshi aliyekuwa mshirika wa karibu wa rais Paul kagame kwenye kundi la lwaasi Rwanda Patriotic Front (RPF), madarakani leo nchini Rwanda, katika harakati za kupigania ukombozi.

Hivi karibuni Rwanda ilishuhudia mdororo wa usalama katika wilaya mbalimbali hasa wilaya ya Rusizi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.