TANZANIA-SIASA-CHADEMA-CCM

Chadema:Waitara alikuwa mzigo

Mwita Waitara wakati huo akiwa mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mkoani Dar es salaam
Mwita Waitara wakati huo akiwa mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mkoani Dar es salaam The citizen

Chama kikuu cha upinzani Tanzania, Chadema kimearifu kuwa aliyekuwa mbunge wake Mwita Waitara alikuwa mzigo kwa chama hicho.

Matangazo ya kibiashara

Waitara aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Ukonga jana alitangaza kujiengua Chadema na kujiunga na chama tawala CCM.

Mwenyekiti wa chadema Wilaya ya Kinondoni, Makongoro Mahanga amenukuliwa na vyombo vya habari vya Tanzania akisema sababu alizotoa  Waitara ni za uongo, kwakuwa tayari chama hicho kilikuwa kwenye mikakati ya kumfukuza.

Mahanga, aliyekuwa naibu waziri wa Wizara mbalimbali katika serikali ya awamu ya nne ameongeza kwamba Waitara alishapewa barua za kufukuzwa na tayari alishany'ang'anywa nafasi zote za kichama.

Wakati akijiunga na CCM jana, Waitara alidai kuwa baadhi ya sababu ni kutofautiana na mwenyekiti Freeman Mbowe baada ya kuhoji kuhusu uchaguzi wa mwenyekiti na masuala yahusuyo ruzuku, ambayo chama hicho kinapokea kutoka kwa msajiri wa vyama vya siasa.