TANZANIA-MALIASILI-USALAMA

Rais wa Tanzania, amtakia kheri waziri wake wa Maliasili alijeruhiwa katika ajali ya gari

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dr Hamis Kigwangala akisaidiwa na wahudumu wa afya wa Hospitali ya Mount meru baada ya kupata ajali mkoani Manyara
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dr Hamis Kigwangala akisaidiwa na wahudumu wa afya wa Hospitali ya Mount meru baada ya kupata ajali mkoani Manyara Mwananchi

Rais wa Tanzania, John Magufuli amemtakia kheri Waziri wa maliasili na utalii wa , Dr. Hamis Andrea Kigwangala amehamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi baada ya kupata ajali ya gari.

Matangazo ya kibiashara

Kigwangala, alijeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea mkoani, Manyara Kakazini mwa Tanzania, akiwa njiani kuelekea Dodoma.

Akizungumza katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Rais Magufuli amesema serikali yake iko bega kwa bega na viongozi hao ambao wamepata ajali wakiwa wanalitumikia taifa.

Katika ajali hiyo Ofisa wa Habari, katika Wizara ya maliasili na utalii, Hamza Temba alipoteza maisha na anazikwa leo kijijini kwao, Hai Mkoani Kilimanjaro.

Viongozi mbalimbali wa kisiasa nchini tanzania wakimwemo Wabunge, Mwigulu Nchemba, Peter Msigwa, Zitto Kabwe wameandika kupitia mitandao ya kijamii wakimtakia kheri waziri Kigwangala ambaye ni mbunge katika Jimbo la Nzega Vijijini Mkoani Tabora.

Katika miezi ya karibuni Tanzania imekumbwa na matukio ya ajali za barabarani katika mikoa ya Mbeya, Kigoma, ajali ambazo zimegharimu maisha ya raia na mali zao.