RWANDA-LA FRANCOPHONE-LOUISE MUSHIKIWABO

Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda aanika vipaumbele vyake, akiwania uongozi La Francophone

Waziri wa mambo ya nje wa Rwnada Louise Mushikiwabo ameweka wzi vipaumbele vinne atakavyovyifanyia kazi endapo atachaguliwa kuwa katibu mkuu muungano wa nchi zinazozungumza lugha ya kifaransa Duniani, La Francophone.

Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo, anawania kuchaguliwa katibu mkuu wa Muungano wa nchi zinazozungumza lugha ya kifaransa.
Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo, anawania kuchaguliwa katibu mkuu wa Muungano wa nchi zinazozungumza lugha ya kifaransa. Ludovic MARIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Akitumia ukurasa wake wa Twitter, Mushikiwabo ametaja vipaumbele hivyo kuwa ni ajira, kuongeza ushawishi wa lugha ya kifaransa duniani, kubadilishana uzoefu na ya mataifa yanayozungumza lugha ya kifaransa duniani.

Kiongozi huyo, amesema vipaumbele vyake vinalenga kutafuta suluhu ya changamoto za pamoja zinazozikabili nchi wanachama wa La Francophone.

Katika uchaguzi huo, Mushikiwabo atachuana na Michaelle Jean raia wa Canada aliyezaliwa nchini haiti.

Jumuiya hiyo yenye nchi 84 inatarajiwa kufanya uchaguzi wake Oktoba 11 na 12, uchaguzi utakaofanyika nchini Armenia.