TANZANIA-IDARA YA UHAMIAJI-USALAMA

Idara ya uhamiaji Tanzania yafafanua kuhusu mikataba kwa raia wanaoishi nje

Idara ya uhamiaji nchini Tanzania, imewataka vijana wanaofanya kazi zisizo na ujuzi nje ya nchi kufika katika ofisi za idara hiyo kuonyesha nakala za mikataba ya kazi na na vibali vya kuishi katika mataifa wanayokwenda kufanya kazi.

Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania, Dr. Ana Makalala
Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania, Dr. Ana Makalala Muungwana.co.tz
Matangazo ya kibiashara

Idara hiyo imesema imeimarisha udhibiti wa kuwazuia kutoka nchini vijana na wasichana wa kitanzania wanaokimbilia ughaibuni kwa madai ya kufanya kazi ambazo hawana ujuzi nazo.

Msemaji wa Idara ya uhamiaji nchini Tanzania, Ally Mtanda amesema utaratibu huo hautawaruhusu watu wengine wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi, kinachotakiwa ni kufuata utaratibu.

“Ifahamike zuio hilo halitawahusu raia wengine wanaokwenda nje ya nchi kwa sababu mbalimbali ilimradi wawe wamekidhi vigezo vya kisheria na na kufuata utaratibu wa kuondoka nchini,”amenukuliwa Mtanda, alipohijiwa na gazeti la kila siku la Mwananchi.

Hatuaa ya Tanzania kuweka mkazo wa kuzuia wasichana na vijana wanaokimbilia nje ya nchi, imekuja miezi kadhaa baada ya kuripotiwa habari za vijana wa kitanzania wanaokimbilia mataifa ya ughaibuni, hususani ya kiarabu, kukumbana na changamoto lukuki zikiwemo za kufanyiwa kazi ngumu na kujiingiza kwenye vitendo viovu.

Hata hivyo suala hilo limeibua mjadala kwenye mitandao yaa kijamii ambapo Rais wa Chama cha wanasheria Tanganyika, Fatma Karume alitoa mtazamo tofaauti.

“Kuna tetesi kwamba watanzania wanaofanya kazi nje ya nchi wanasimamishwa na uhamiaji kurudi kazini bila vibali kutoka serikalini.Mwaka jana tu wakenya wanaofanya kazi nje ya nchi wamepeleka dola bilioni 1.95 kwao.Kenyans wanaexport hizo services. Sisi hapa tunatakazana,”