KENYA-NDEGE-UKUNGU

Ukungu watatiza safari za ndege jijini Nairobi nchini Kenya

Hali ya ukungu katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, Agosti 10 2018
Hali ya ukungu katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, Agosti 10 2018 KenyaAirports

Safari za ndege kutoka na kwenda katika Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, huenda zikacheleweshwa kwa sababu ya hali mbaya ya hewa katika jiji hilo.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka ya safari za ndege nchini humo KAA imesema kuna ukungu mwingi ambao unachelewesha kutua na kuondoka kwa ndege zinakwenda ndani na nje ya nchi hiyo.

Ukungu hutatiza rubani kuwa na uwezo wa kuona kwa makini na hivyo, inaweza kusababisha ajali.

“Kutokana na ukungu mwingi unaoshudiwa jijini Nairobi, kuna uwezekano wa kucheleweshwa kuondoka kwa ndege au zikaelekezwa kwingine,"

"Tafadhali wasiliana na Shirika la ndege unatarajia kusafiri nalo kupata taarifa zaidi, “ tangazo la Mamlaka hiyo limeripotiwa katika ukurasa wake wa Twitter.

Hali hii pia imeathiri uwanja mwingine wa ndege ule wa Wilson ambao hupokea ndege ndogo zinazofanya safari nchini humo.

Hii ni mara ya pili kwa hali hii, kushuhudiwa katika uwanja huo mkubwa katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki.