BURUNDI-MAZINGIRA

Burundi yatangaza muda wa mwisho wa kutumia mifuko ya plastiki

Kutokana kusudio hilo, serikali imetangaza kutoa muda kwa walioajiriwa, kujiajiri na kuwekeza kwenye biashara ya mifuko ya plastiki kujiandaa kuacha shughuli hiyo na kujikita kwenye utengenezaji wa vifungashio mbadala.
Kutokana kusudio hilo, serikali imetangaza kutoa muda kwa walioajiriwa, kujiajiri na kuwekeza kwenye biashara ya mifuko ya plastiki kujiandaa kuacha shughuli hiyo na kujikita kwenye utengenezaji wa vifungashio mbadala. © RFI/Altin Lazaj

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ametoa amri inayopiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki nchini humo na kutoa muda wa mwisho wa kutumia mifuko hiyo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja na nusu, kulingana na agizo la rais.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa amri hiyo iliyosainiwa na Rais Nkurunziza utengenezaji, uagizaji, kuhifadhi, uuzaji na matumizi mengine ya mifuko ya plastiki vitapigwa maarufuku kufikia kipindi hicho.

Aidha amri hiyo itatoa ruhusa maalum ya mifuko ya plastiki na malighafi nyingine za plastiki kutumika katika huduma za ufungishaji dawa katika viwanda nchini humo kwa lengo la kukabiliana na uaharibifu wa mazingira

"Kipindi cha miezi 18 kinatolewa, kuanzia baada rais kutia saini nakala hii, ili kuweza kuuza na kutumia mifuko ya plastiki iliyokuwa imehifadhiwa na ile ambayo ilikua iliagizwa nje ya nchi," nakala hiyo imebaini.

Lakini mifuko ya plastiki, vifaa vya plastiki vinavyotumiwa katika huduma za matibabu, katika viwanda na maduka ya dawa" vitaendelea kutumiwa kwa masharti, imeongeza nakala hiyo.

Nchi nyingine za Afrika tayari zimeanza kupikabiliana na uchafuzi wa vifaa na mifuko ya plastiki, kama vile Morocco, Rwanda na Kenya, ambazo zilipiga marufu matumizi ya mifuko ya plastiki.