UGANDA-HAKI-USALAMA-SIASA

Bobi Wine ashtakiwa kwa madai ya uhaini Uganda

Bobi Wine atoa ishara kwa wafuasi wake kuwa wakati umewadia. Kauli mbiu ya kampeni yake, "sawa". Julai 11, 2017.
Bobi Wine atoa ishara kwa wafuasi wake kuwa wakati umewadia. Kauli mbiu ya kampeni yake, "sawa". Julai 11, 2017. RFI / Charlotte Cosset

Mbunge wa Uganda na mwanamuziki nguli Robert Kyagulanyi, anayejulikana kwa jina la Bobi Wine, anatarajiwa kufukishwa katika mahakama ya kijeshi kwa madai ya kumiliki silaha kinyume cha sheria baada ya kukamatwa kwake.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa polisi, Robert Kyagulanyi alikuwa na silaha mbili, kosa ambalo anatakiwa kufikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi kulingana na sheria ya Uganda.

Msemaji wa jeshi Richard Karemire amesema Bw Kyagulanyi atafikishwa "mbele ya mahakama ya kijeshi" huko Gulu, kaskazini mwa Uganda.

Kyagulanyi haijaonekana hadharani tangu kukamatwa kwake Jumanne wiki hii, amesema mwanasheria wake Asuman Basalirwa. "Jeshi halijaturuhusu tumuone, hata familia yake haijamuona," amesema.

Bobi Wine alikamatwa katika mji wa Arua, kaskazini magharibi mwa Uganda, ambako alikuwa akiendesha kampeni kwa mgombea wa upinzani katika uchaguzi mdogo ulio kuwa na ushindani mkubwa, ambapo rais Yoweri Museveni aliamua kuwasili katika mji huo kumuunga mkono mgombea wa chama tawala.

Bw Kyagulanyi alikamatwa kwa kosa la kuzuia msafara wa magari ya rais, msemaji wa polisi ameongeza.

Katika makabiliano na wafuasi wa upinzani, polisi walifyatua risasi hovyo kwa kuwatawanya waandamanaji, na kumuua dereva wa Bobi Wine.

Kwenye ukurasa wake wa Twitter, kabla ya kukamatwa kwake, Bw Kyagulanyi alidai kuwa kifo cha dereva wake kilitokea tu baada ya polisi kuchanganyikiwa wakidhani kuwa walimua yeye. "Polisi wamlipiga risasi dereva wangu wakifikiri kuwa ni mimi," alisema Bw Kyagulanyi.