UGANDA-MAUAJI-USALAMA

Mtu moja auawa katika makabiliano kati ya wafuasi wa upinzani na polisi Uganda

Bobi Wine atoa ishara kwa wafuasi wake kuwa wakati umewadia. Kauli mbiu ya kampeni yake, "sawa". Julai 11, 2017.
Bobi Wine atoa ishara kwa wafuasi wake kuwa wakati umewadia. Kauli mbiu ya kampeni yake, "sawa". Julai 11, 2017. RFI / Charlotte Cosset

Mtu mmoja ameuawa na wengine watano kujeruhiwa katika mji wa Mityana baada ya polisi siku ya uJmapili kukabiliana na wafuasi wa mbunge wa upinzani Francis Zaake, baada ya ripoti kuwa hali yake ya afya ni mbaya.

Matangazo ya kibiashara

Zaake ni mmoja wa wanasiasa wa upinzani waliokamatwa na kuzuiwa na wanajeshi katika mji wa Arua wiki iliyopita, baada ya kutoka kwa machafuko ya kisiasa na msafara wa rais Yoweri Museveni kurushiwa mawe.

Wanasiasa hao wanadaiwa kupigwa na kujeruhiwa vibaya na wanajeshi baada ya kukamatwa, akiwemo Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine ambaye amezuiwa kwenye kambi ya jeshi.

Kyagulanyi ni mwanasiasa mwenye umri wa miaka 36 ambaye umaarufu wake unaelezwa na wachambuzi wa siasa kuwa unampa tumbo joto rais Yoweri Kaguta Museveni na mwanasiasa mkongwe wa upinzani Kizza Besigye.