UGANDA-USALAMA

Jeshi la Uganda laomba radhi baada ya mwandishi wa habari kupigwa

Wafuasi wa mwanasiasa wa Uganda Robert Kyagulanyi, anayefahamika kwa jina la Bobi Wine, ambaye alikamatwa hivi karibuni, wakichoma moto matairi na hivyo kuzuia shughuli katika ya mji mkuu, Kampala, Uganda Agosti 20 2018.
Wafuasi wa mwanasiasa wa Uganda Robert Kyagulanyi, anayefahamika kwa jina la Bobi Wine, ambaye alikamatwa hivi karibuni, wakichoma moto matairi na hivyo kuzuia shughuli katika ya mji mkuu, Kampala, Uganda Agosti 20 2018. STRINGER / AFP

Jeshi la Uganda limeomba radhi, baada ya maafisa wake kumpiga na kumjeruhi mpigapicha wa Shirika la Habari la Reuters James Akena siku ya Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

Akena ni miongoni mwa wanahabari walioshambuliwa na wanajeshi wakati wa maandamano ya kushinikiza kuachiliwa huru kwa mbunge wa upinzani Robert Kyagulanyi anayezuiwa na jeshi.

Taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi, ilieleza kuwa kitendo hicho kilichofanywa na askari wake kuwa si cha weledi na kusema kuwa watakamatwa kwa mujibu wa sheria za jeshi nchini humo.

Kumekuwa na mvutano wa kisiasa nchini Uganda baada ya mbunge Bobi, na wabunge wanne wa upinzani, kukamatwa wiki iliyopita.

Bw Kyagulanyi anatarajiwa kufikishwa tena katika Mahakama ya kijeshi kesho baada ya kufunguliwa mashtaka ya kumilki siaha nkinyume na sheria.

Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Kenya wamepanga maandamano Alhamisi wiki hii jijini Nairobi kuungana na wafausi wa mbunge huyo kushinikiza kuachiliwa kwake.