TANZANIA-BURUNDI-USALAMA-HAKI

Tanzania yashtumiwa kuwafanyia vitisho wakimbizi wa Burundi

Baada ya miaka mitatu ya mgogoro wa kisiasa nchini Burundi, Tanzania imekuwa ni nchi katika bara la Afrika, inayowapa hifadhi wakimbizi wengi wkutoka Burundi.

Des réfugiés burundais de retour de Tanzanie, dans un camp de transit en novembre 2012, espèrent être réinstallés à Musenyi, dans le sud du Burundi.
Des réfugiés burundais de retour de Tanzanie, dans un camp de transit en novembre 2012, espèrent être réinstallés à Musenyi, dans le sud du Burundi. AFP/TONY KARUMBA
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya wakimbizi hao nchini tanzania imefikia sasa zaidi ya 400,000 ambao wametawanywa katika kambi mbalimbali za wakimbizi. Wengine wametawanyika katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Rwanda na Uganda.

Shirika lisilo la kiserikali la International Refugee Right Initiative (IRRI) limeishtumu serikali ya Tanzania likisema kuwa imekua ikitoa shinikizo na vitisho kwa wakimbizi wa Burundi waishio nchini humo ili waweze kurejea nchini mwao. Mmoja wa viongozi wa shirika hilo, Thijs Van Laer, amelaani vikwazo vinavyowekwa na viongozi wa Tanzania ili kupunguza shughuli za kiuchumi, pamoja na hatua nyingine.

Wakimbizi wa Burundi wanapopatikana nje ya kambi, wanakamatwa na mara nyingi hupigwa na maafisa wa usalama wa Tanzania.

Thijs Van Laer amesema serikali ya Tanzania ina ushirikiano tosha na serikali ya Burundi kwa kuwafanyia vitisho wakimbizi wa Burundi ili waweze kurudi nyumbani.

Serikali ya Tanzania haijazungumza chochote kuhusiana na madai hayo.