KENYA-UCHUMI

Ukaguzi waonyesha kupotea kwa shilingi Bilioni 1.7 kutoka wizara ya michezo Kenya

Mji mkuu wa Kenya Nairobi, ambako sakata la kuwashughulikia watu wanaojihusisha na kashfa za rushwa na ufisadi linaendelea.
Mji mkuu wa Kenya Nairobi, ambako sakata la kuwashughulikia watu wanaojihusisha na kashfa za rushwa na ufisadi linaendelea. Yasuyoshi CHIBA / AFP

Ripoti ya mkaguzi mkuu wa fedha nchini Kenya inaonesha kuwa Shilingi za nchi hiyo Bilioni 1.7, hazijatolewa ufafanunuzi kuhusu namna zilivyotumiwa kuandaa mashindani ya ridha ya dunia chini ya miaka 20 mwaka uliopita.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja ikiwa ni mwezi mmoja tu baada ya shirikisho la mashindano ya riadha duniani IAAF kuipa Kenya nafasi ya kuwa mwandaaji wa mbio za vijana chini ya umri wa miaka 20 mwaka 2020

Serikali ilitenga Shilingi bilioni 3.5 kusadia katika maandalizi ya mashindano hayo makubwa lakini imebainika kuwa kuna fedha zilizotoweka.

Kwa mujibu wa Mkaguzi wa hesabu za serikali, Edward Ouko, Serikali ilitoa kiasi ya shilingi bilioni 3.5 kwa ajili ya mashindano lakini pesa halisi iliyotumika kihalali ni shilingi bilioni 1.8 na kukiwa hakuna taarifa kuhusu bilioni 1.7, lakini pia kukiwa na deni linalopaswa kulipwa la shilingi milioni 138.

Katibu mkuu wa wizara ya michezo ya Kenya, Kirimi Kaberia amesema hatua zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria baada ya mapitio ya ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali.

Hii ni mara ya pili kunatokea ufisadi katika pesa za michezo kwa vijana nchini Kenya.

Miaka 40 iliyopita, wakati Kenya ilipoandaa mashindano ya Afrika, kiasi cha Milioni 60 za nchi hiyo pia zilipotea.

Hii ni kashfa mpya inayokuja wakati huu serikali ya rais Uhuru Kenyatta ikiendelea kukabiliana na ufisadi