UGANDA-YOWERI MUSEVENI-BOBI WINE

Bobi Wine aachiliwa huru na kukamatwa tena nchini Uganda

Mwanasiasa wa Upinzani nchini uganda Robert Kyagulanyi maarufu kwa jina la Bobi Wine
Mwanasiasa wa Upinzani nchini uganda Robert Kyagulanyi maarufu kwa jina la Bobi Wine The Standard

Mwanasiasa wa upinzani na mbunge wa Kyadondo Mashariki, Robert Kyagulani, maarufu kama Bobi Wine amekamatwa na Jeshi la polisi, muda mfupi baada ya kuachiliwa huru na mahakama ya kijeshi.

Matangazo ya kibiashara

Akiambatana na wakili na familia yake Bobi Wine amepelkwa na ktika mahakama ya hakimu mkazi ya Gulu na ripoti zinasema huenda akafunguliwa mashtaka ya uhaini.

Wakati akitoka mahakama mbunge huyo alionekana kuwa mchovu na akitembelea gongo, hatua inayooibua madai kuwa alipigwa na vikosi vya usalama.

Mawakili wake wameapa kupambana kuhakikisha mwanasiasa huyo anapata dhamana ili akapatiwe matibabu.

Wakati huohuo, mwanasiasa wa upinzani Dr. Kiiza Besigye,amekamatwa na vyombo vya usalama na anashikiliwa katika kituo cha Polisi cha Naggalama.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Dr. Besigye aliarifu kuwa mapema leo maofisa wa polisi walizingira nyumba yake, wakilenga kumzuia asihudhurie kesi ya Bobi Wine.