UGANDA-USALAMA-HAKI

Bobi Wine kufikishwa mahakamani Alhamisi hii Uganda

Mwanamuziki na mwanasiasa Bobi Wine wakati wa maandamano huko Kampala Julai 11, 2018.
Mwanamuziki na mwanasiasa Bobi Wine wakati wa maandamano huko Kampala Julai 11, 2018. Isaac Kasamani / AFP

Mbunge wa upinzani Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, anatarajiwa kufikishwa katika Mahakama ya kijeshi hivi leo. Wakili wa Bobi Wine anasema kuwa mteja wake ameteswa sana na jeshi, lakini jeshi kwa upande wao wanakataa kumtesa.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa, kesi dhidi ya mbunge huyo itafanyika mjini Gulu na sio jijini Kampala kwa sababu za kiusalama, wakati huu maandamano yakitarajiwa kushinikiza kuachuliwa kwake huru pamoja na wanasiasa wengine wanne. Maandamano kama hayo yanatarajiwa kufanyika jijini Nairobi nchini Kenya.

Zaidi ya wasanii 80 wanataka Bobi wine aachiwe huru mara moja wakiwemo wasanii maarufu kama Chris Martin, Angelique Kidjo na Damon Albarn.

Bobi Wine anatarijiwa kufikishwa mahakamani juu ya madai ya kumiliki silaha kinyume na sheria.

Wakati huo huo, wanahabari nchini Uganda wanaendelea kukabiliwa na wasiwasi baada ya kupigwa wiki hii na wanajeshi na Polisi.

Mtandao wa haki za binadamu za wanahabari nchini Uganda umetoa saa 48 kwa jeshi kuwatambulisha askari wake waliowajumu wanahabari.