BURUNDI-UNSC-USALAMA-SIASA

Burundi yaendelea kupata shinikizo kuelekea uchaguzi wa 2020

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza (Kushoto) ambaye hivi karibuni alitangaza kuwa hatowania katika uchaguzi wa mwaka 2020 na mkewe Denis Nkurunziza.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza (Kushoto) ambaye hivi karibuni alitangaza kuwa hatowania katika uchaguzi wa mwaka 2020 na mkewe Denis Nkurunziza. STR / AFP

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekosoa mwendo wa mazungumzo ya kisiasa nchini Burundi, licha ya rais Pierre Nkurunziza kusema kuwa hatawania tena urais mwaka 2020.

Matangazo ya kibiashara

Baraza hilo limekaribisha hatua hiyo ya rais Nkurunziza lakini linataka mazungumzo hayao kuedelea kwa haraka na suluhu kupatikana, ili kuwezesha Uchaguzi utakaokuwa huru na haki baada ya miaka miwili.

Mazungumzo ya kisiasa nchini Burundi yanaongozwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki, na hadi sasa hakuna mwafaka uluofikiwa kati ya serikali na upinzani.

Upinzani umekua ukikosoa mwenendo wa muwezeshaji wa mazungumzo hayo, rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa, ukisema kwamba anaegemea upande wa serikali ya Burundi.

Hivi karibuni serikali ya Burundi imetangaza kwamba haitorudi kutuma wajumbe wake katika mazungumzo yatakayofanyika nje ya nchi, ikitaka mazungumzo hayo yaendelea nchini Burundi.