ETHIOPIA-ABIY AHMED-UCHUMI

Benki ya dunia kuipatia Ethiopia msaada wa kibajeti wa dola bilioni moja

Waziri Mkuu wa  Ethiopia, Abiy Ahmed akihutubia bunge ,tarhe 19 April 2018.
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed akihutubia bunge ,tarhe 19 April 2018. REUTERS/Tiksa Negeri/File Photo

Benki ya dunia (WB) itaipitia Ethiopia msaada wa kibajeti unaokisiwa kufikia dola bilioni moja, Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abiy Ahmed ameambia vyombo vya habari.

Matangazo ya kibiashara

Miaka mitatu iliyopita Benki ya dunia na mashirika ya wahisani yalithitisha misaada ya kibajeti kwa taifa hilo la Afrika mashariki, baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 uliogubikwa na ukiukwaji wa taratibu.

Waziri Mkuu Ahmed amesema hatua ya benki ya dunia inakuja kufuatia mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa yanayotekelezwa na utawala wake.

Katika kutilia mkazo mabadiliko yanayochukuliwa na utalawa wake, Ahmed ambaye pia ni kiongozi wa chama tawala cha Ethiopian Peoples Revulutionary Democratic Front (EPRDF) amearifu kuwa chama hicho kiko tayari kuandaa uchaguzi huru na wa haki mwaka 2020.

Tangu alipochukua madaraka miezi kadhaa iliyopita kutoka kwa mtangulizi wake, Hailemariam Desalegn,Abiy Ahmed mwenye umri wa miaka 42 amerejesha uhusiano wa kidipolomasia na Eritrea na kutekeleza mageuzi kadhaa ambayo yamepigiwa upatu na nchi za Afrika na jumuiya ya kimataifa.