Jukwaa la Michezo

Mwelekeo wa soka la vijana Afrika Mashariki na kati baada ya kutamatika kwa michuano ya kufuzu fainali za Afrika Jijini Dar es salaam

Imechapishwa:

Michuano ya kufuzu fainali za Afrika kwa vijana chini ya miaka 17, kanda ya Afrika Mashariki na Kati zimefikia tamati Jijini Dar es salaam, Tanzania kwa Uganda kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ethiopia na kuungana na Tanzania kucheza fainali zitakazochezwa mwaka 2019 nchini Tanzania.Je uamuzi wa kuchezwa mechi za mchujo katika kanda ulikuwa sahihi na nini hatima ya soka la vijana katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati? Fredrick Nwaka ameungana na wachambuzi Samuel John na Ali Saleh kutathimini kwa kina.

Wachezaji wa Timu ya Vijana ya Uganda wakishangilia baada ya kufuzu kucheza fainali za Afrika, zitakazofanyika mwakani nchini tanzania
Wachezaji wa Timu ya Vijana ya Uganda wakishangilia baada ya kufuzu kucheza fainali za Afrika, zitakazofanyika mwakani nchini tanzania Twitter/Fufa