TANZANIA-BUNGE LA TANZANIA-HAWA GHASIA

Hawa Ghasia ajiuzulu uenyekiti wa kamati ya bajeti ya Bunge la Tanzania

Hawa Ghasia, Mbunge wa Jimbo la Mtwara VijijinI, Kusini mwa Tanzania
Hawa Ghasia, Mbunge wa Jimbo la Mtwara VijijinI, Kusini mwa Tanzania Mwananchi

Mwenyekiti wa kamati ya bajeti ya bunge la Tanzania Hawa Ghasia, amejiuzulu wadhifa wake hii leo, ripoti za vyombo vya habari vya Taanzania, zimearifu.

Matangazo ya kibiashara

Kujiuzulu kumekuja siku chache kabla ya bunge la Tanzania kuanza vikao vyake Mjini Dodoma, vikao vya bunge hilo vinatazamiwa kuanza Septemba 4.

Ripoti zilizochapishwa na Mtandao wa gazeti la Mwananchi la Tanzania, zinasema Ghasia ambaye ni mbunge wa Jimbo la Uchaguzi la Mtwara Vijijini ameng'atuka sanjari na makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Jitu Soni ambaye ni mbunge wa Jimbo la Uchaguzi la Babati Vijijini.