TANZANIA-KANGI LUGOLA-JESHI LA POLISI

Kangi Lugola aapa kuwachukulia hatua askari wanaobambikia kesi wananchi

Waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania, Kangi Lugola amearifu kwamba atawachukulia hatua askariu wa jeshi watakaohusika kubambikizia kesi wananchi. 

Waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania, Kangi Lugola
Waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania, Kangi Lugola East Africa Television (EATV)
Matangazo ya kibiashara

Aidh, kiongozi huyo amesema ataendelea kuwaweka mahabusu askari wa jeshi hilo wanaokiukwa taratibu.

Siku chache zilizopita, Lugola alimuweka mahabusu Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara Mjini, Ibrahim Mhando na hii leo kiongozi huyo ameviambia vyombo vya habari Mjini Dar es Salaam ameonye hatua ya askari wa jeshi hilo kubambikizia kesi wananchi.

'Nimeanza kutembelea vituo vya polisi, nimesema hakuna kituo cha polisi ambacho sitafika ili nijionee utendaji wa polisi na namna wananchi wanavyohudumiwa,"amunukuliwa kiongozi huyo katika mtandao wa gazeti la kila siku la Mwananchi.

Tangu alipoteuliwa na rais wa Tanzania kuongoza Wizara ya mambo ya ndani, akichukua nafasi ya Dr. Mwigulu Nchemba aliyefutwa kazi, Waziri Lugola amekuwa akitoa matamko ya mara kwa mara ya watendaji walio chini ya wizara yake.