KENYA-UHURU KENYATTA-RUSHWA

Naibu Jaji Mkuu wa Kenya, akamatatwa kwa tuhuma za rushwa

Naibu Jaji Mkuu wa Kenya, Jaji Philomena Mwilu amekamatwa leo Agosti 28 mwaka 2018
Naibu Jaji Mkuu wa Kenya, Jaji Philomena Mwilu amekamatwa leo Agosti 28 mwaka 2018 citizentv.co.ke

Mwendesha mashtaka mkuu wa Serikali ya kenya, Noordin Haji amethibitisha kukamatwa kwa Naibu Jaji mkuu wa Kenya, Jaji Philomena Mwilu.

Matangazo ya kibiashara

Jaji mwilu alikamatwa leo mchana akituhumiwa kujihusisha na rushwa. Kukamatwa kwa kiongozi huyo mwenye cheo cha pili katika mahakama nchini Kenya.

Katika taarifa yake iliyochapishwa na gazeti la Daily Nation la Kenya, imemnukuu Noordin Haji.

'Katika kipindi cha mwezi mmoja kumekuwa na kilio cha kupambana na ufisadi na mgogoro wa kiuchumi katika nchi yetu ambayo inaathiri maisha ya wananchi na maendeleo ya nchi yetu,"

Rais Uhuru Kenyatta, katika siku za karibuni ameapa kupambana na ufisadi na rushwa nchini Kenya, akiapa kuwa yu tayari kupoteza marafiki katika vita hiyo.