Habari RFI-Ki

Mkataba wa mwisho wa amani watiwa saini nchini Sudan Kusini

Sauti 10:12
Kiongozi wa waasi Riek Machar (Kushoto) akiwa na rais Salva Kiir (Kulia ) wakitia mkataba wa amani jijini Khartoum nchini Sudan
Kiongozi wa waasi Riek Machar (Kushoto) akiwa na rais Salva Kiir (Kulia ) wakitia mkataba wa amani jijini Khartoum nchini Sudan REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Je, amani ya kudumu inakuja nchini Sudan Kusini ? Hatimaye, rais Salva Kiir na hasimu wake Riek Machar wametia saini mkataba wa mwisho wa amani baada ya mazungumzo ya miezi kadhaa jijini Khartoum nchini Sudan, ambao pamoja na mambo mengine, unasitisha vita na kuwezesha kuundwa kwa serikali ya pamoja, huku Machar akitarajiwa kurejea kama Makamu wa kwanza wa rais.