UGANDA-YOWERI MUSEVENI-BOBI WINE

Bobi Wine aelekea Marekani, kupokea matibabu

Mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda, Bobi Wine
Mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda, Bobi Wine BBC

Vyombo vya usalama nchini Uganda, vimemrhusu mwanasiasa wa upinzani Robert Kyagulanyi kuondoka nchini humo na kwenda nchini Marekani kupokea matibabu.

Matangazo ya kibiashara

Ofwono Opondo, msemaji wa serikali ya Uganda awali alieleza kwamba Kyagulanyi, maarufu kwa jina la Bobi Wine alizuiliwa kuondoka nchini uganda, kwa kuwa huenda alikuwa akiimkimbia nchi hiyo.

Hata hivyo jana usiku Mbunge huyo wa Kyadondo Mashariki aliruhusiwa kuondoka nchini Uganda baada ya mkutano wa dharura wa bodi ya madaktari.

Video iliyorushwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii inamuonyesha Bobi Wine akifanyiwa ukaguzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe, kabla ya kuondoka nchini Uganda.

Bobi WIne sanjari na wabunge wengine wa upinzani nchini Uganda, inaelezwa wanatuhumiwa kwa kosa uhaini kwa kushambulia msafara wa rais Museveni wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo, alikamatwa na kushikiliwa katika kambi ya kijeshi kabla ya kuachiwa na kukamatwa tena na polisi.

Kukamatwa kwa mwanasiasa huyo kumezua sintofahamu ya kisiasa nchini Uganda ambapo mara kadhaa vyombo vya usalama vimekabiliana na wafuasi wa upinzani, wanaopinga kukamatwa kwa Bobi Wine na wabunge wengine wa upinzani.