BURUNDI-SIASA-ICG-PIERRE NKURUNZIZA

ICG: Uchumi wadhoofishwa na mgogoro wa kisiasa Burundi

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza REUTERS/Evrard Ngendakumana

Shirika la Kimataifa linalotatua migogoro International Crisi Group (ICG) limeonya kuwa mdororo wa uchumi wa Burundi unasababishwa na mgogoro wa kisiasa na usalama unaondelea kwa miaka mitatu nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Mgogoro huo umerudisha nyuma maendeleo ya nchi hiyo hasa katika sekta ya kijamii na kiuchumi yaliyofanywa kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita, ICG imebaini.

"Ingawa kura ya Ndiyo iliyoshinda wakati wa kura ya maoni kuhusu mageuzi ya Katiba Mei 17, 2018 imefungua awamu mpya katika mgogoro wa sasa wa kisiasa na usalama nchini Burundi, kushuka kwa uchumi kunaongeza hatari ya kuzuka kwa machafuko," ICG imeandika katika ripoti yake.

Nchi imeongezeka kutoka ukuaji wa wastani wa asilimia 4.2 kwa kipindi cha mwaka 2004-2014 kwa uchumi kushika kwa kiwango cha 3.9% mnamo mwaka 2015 na 0.6% mnamo mwaka 2016.

"Maendeleo ya kiuchumi na ya kijamii yaliyofanywa katika miaka ya 2000" sasa yako hatarini wakati mdororo wa kiuchumi umeibuka, " ICG imeongeza.

"Ili kuendelea kuishi, Warundi wengi wanatumia njia isiyo halali kwa kutafuta ajira ya nyingine ya kukidhi mahitaji yao, ikiwa ni pamoja na kujihusisha na rushwa au kuondoa gharama zote zisizo muhimu." "Wakati huo makundi mbalimbali ya raia wanakiona cha mtima kuni," ripoti hiyo imeelezea.

"Muongo mmoja wa maendeleo katika sekta ya afya na elimu umekwenda kombo: madaktari wengi waliitoroka nchi, mara nyingi walimu hawapati mishahara yao na elimu ya juu inakabiliwa na mambo mbalimbali" , ripoti hiyo imeongeza.

Ripoti hiyo inasema kuwa mwaka 2017, Burundi ilikuwa na madaktari 500 tu kwa wakaazi zaidi ya milioni 11.

Burundi imekuwa katika mgogoro tangu Rais Pierre Nkurunziza alipotangaza mnamo mwezi Aprili 2015 kuwa atawania muhula wa tatu uliozua utata na baadaye alichaguliwa tena Julai mwaka huo huo.

Machafuko nchini Burundi yamesabbabisha vifo vya watu 1,200, na watu zaidi ya 400,000 kati ya mwezi Aprili 2015 na mwezi Mei 2017 waliyahama makazi yao, kulingana na makadirio ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ambayo imeanzisha uchunguzi nchini humo.

Mageuzi ya Katiba yaliyopitishwa mnamo mwezi Mei kwa kura ya maoni yalifungua uwezekano kwa rais Pierre Nkurunziza, madarakani tangu mwaka 2005, kuwania kwa mihula miwili ya mika saba kila muhula kuanzia mwaka 2020. Lakini alishangaa watu wengi kwa kutangaza mwezi Juni kuwa hatowania katika uchaguzi wa urais mwaka 2020.