TANZANIA-HAKI ZA BINADAMU

LHRC: Vitendo vya ubakaji wa watoto vyaongezeka Tanzania

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania, LHRC Anna Henga
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania, LHRC Anna Henga Dar24

Kituo cha sheria na haki za Binadamu Tanzania (LHRC) kimetoa ripoti ya nusu mwaka kuhusu mwenendo wa haki za binadamu nchini Tanzania na kuarifu ongezeko la vitendo vya ubakaji nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo wa mwaka 2018 watoto 2365 walibakwa, takwimu ambazo ni s awa na watoto 394 kwa siku.

Ripoti hiyo inasema katika kipinidi cha miezi sita ya kwanza kwa mwaka 2018 matukio ya ukatili kwa watoto yaliyoripotiwa ni 6376 na matukio ya 2365 yakitokana na ubakaji.

Idadi hiyo imeongezeka maradufu, ikilinganishwa na ripoti ya nusu mwaka ya mwaka jana ambayo ilionyesha watoto 759 walibakwa.

Akiwasilisha ripoti hiyo mtafiti wa Kituo cha sheria na haki za binadamu Tanzania, Fundikira Wazambi amepasha kwamba vitendo hivyo mara nyingi hufanywa na ndugu wa karibu na majirani.

Kuchapishwa kwa ripoti hiyo kunakuja wakati matukiuo ya ukatili wa wanawake na watoto yakiripotiwa katika mataifa mbalimbali barani Afrika.

Hata hivyo, utandawazi na mmomonyoko wa maadili unatajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazochochea vitendo cha ukatili katika jamii.