RWANDA-SIASA

Rwanda: Upinzani kushiriki vikao vya Bunge

Frank Habineza, kiongozi wa chama cha Green Party nchini Rwanda.
Frank Habineza, kiongozi wa chama cha Green Party nchini Rwanda. Rwandagreendemocrats.org

Chama kimoja cha upinzani nchini Rwanda kinatarajia kushiriki vikao vya Bunge la nchi hiyo baada ya uchaguzi wa Jumatatu wiki hii, kulingana na matokeo ya awali yaliyotolewa Jumanne Septemba 4, 2018.

Matangazo ya kibiashara

Chama cha Green Party cha Frank Habineza kilipata 5% ya kra katika uchaguzi wa wabunge ulifanyika Jumatatu wiki hii, sawa na kiwango cha chini kinachohitajika kushiriki kuwa na viti bungeni, kulingana na matokeo yaliyotangazwa Jumanne wiki hii na Tume ya Uchaguzi nchini humo.

Ushindi wa chama hicho cha upinzani sio pingamizi kwa Rais Paul Kagame na chama chake cha RPF.

Kwa ushindi huo, chama cha Green Party kitakua na viti viwli bungni.

Uchaguzi huo ulihusu viti hamsini na tatu kati ya viti 80 vinavyohitajika bungeni. Viti 27 vinavyosalia vimetengewa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, ambao huchaguliwa na Halmashauri maalum, kamati na mashirika.

Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutangazwa Septemba 16.

"Hii ni ishara kwamba Rwanda inafungua wigo wake wa kisiasa," amesema Frank Habineza, mwanachama wa zamani wa RPF ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa sera za Paul Kagame, na ambaye amefutilia mbali taarifa zinazosema kwamba ni mpinzani-mshirika wa Paul Kagame. "Tumefikia lengo kubwa kwa kupata viti katika Bunge", amesema Bw Habineza.

Muungano unaoongozwa na RPF umeshinda asilimia 74 ya kura (sawa na viti 40), kiwango kidogoikilinganishwa na uchaguzi wa miaka 5 iliyopita. Vyama vitatu vinavyounga mkono sera ya serikali vinatarajia kugawana viti vinavyobaki.