UGANDA-SANAA

Serikali ya Uganda yapiga marufuku tamasha la muziki

Simon Lokodo, Waziri wa Maadili wa Uganda, apiga marufuku Nyege Nyege, moja yatamasha kubwa la muziki za Afrika Mashariki, Kampala, Uganda, Septemba 4, 2018.
Simon Lokodo, Waziri wa Maadili wa Uganda, apiga marufuku Nyege Nyege, moja yatamasha kubwa la muziki za Afrika Mashariki, Kampala, Uganda, Septemba 4, 2018. Uganda Media Centre/Twitter.com

Serikali ya Uganda imepiga marufuku mojawapo ya tamasha kubwa la muziki wa Afrika Mashariki, ikisema itakua kuendeleza msuala ya ngono, ushoga, na vitendo vingine ambavyo inaona kuwa ni ukiukwaji wa maadili, waziri wa Maadili, Simoni Lokodo ametangaza.

Matangazo ya kibiashara

"Baada ya kuchunguza ukweli wote (...), tamasha hilo limepigwa marufuku," amesema Waziri Lokodo katika taarifa yake, akielezea kuwa uamuzi huu ulichukuliwa baada ya kukutana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mkuu wa majeshi na Mkuu wa Polisi.

Tamasha hiyo, ambayo ilikuwa ilipangwa kiufanyika Septemba 6 hadi 9, "ilipangwa ili kufanya sherehe ya ushoga na mambo mengine yanayokiuka maadili (LGBT), miongoni mwa wengine, pamoja na kuajiri vijana kwa vitendo hivi potofu", ameongeza waziri.

Akinukuliwa kwenye akaunti ya Twitter ya idara ya mawasiliano ya serikali ya Uganda, Lokodo amesema kuwa "kutakuwa na uchafu na vitendo vya ngono wakati wote, kutafanyika vitendo vya ngono hadharani."

"Ni bahati mbaya kufuta Nyege Nyege katika dakika ya mwiho, lakini hatuwezi kukubali kupoteza maadili yetu, ushoga hautakubalika," amesema waziri Lokodo, akibaini kuwa tamasha linaloungwa mkono na shetani haikubaliki Uganda".

"Jina la tamasha lenyewe linatisha, lina maana + ngono, ngono +," amesema waziri huyo ambapo watu 10,000 walikuwa wanatarajiwa kwenye tamasha hilo, ikiwa ni pamoja na watalii wengi wa kigeni. "Nilitaka kupiga marufuku Nyege Nyege mwaka jana, lakini lilifanyika kwa bahati mbaya tu", amesema waziri Lokodo

Katika lugha ya Uganda, "Nyege Nyege" inamaanisha "haja ya kushindwa kucheza", lakini maneno

haya yanatafsiri vitendo vya ngono katika lugha nyingine za kanda hii, waziri wa Uganda wa maadili ameongeza.

"Wageni hawatakuja Uganda kwa ngono," amesema Lokodo, pia akimaanisha kuwepo kwa pombe na madawa ya kulevya yaliyopigwa marufuku. "Ni lazima tuokoe picha ya nchi hii" amebaini waziri Lokodo.