RWANDA-MAUAJI YA KIMBARI

Mauaji ya kimbari: Watu watano wakamatwa wakijaribu kutoa rushwa Rwanda

Mwanasheria Cecil John Maruma na mteja wake Augustin Ngirabatware, aliyekuwa waziri wa mipango ya mijini wa Rwanda, wakati wa kesi yake ikisikilizwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Arusha, Oktoba 10, 20
Mwanasheria Cecil John Maruma na mteja wake Augustin Ngirabatware, aliyekuwa waziri wa mipango ya mijini wa Rwanda, wakati wa kesi yake ikisikilizwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Arusha, Oktoba 10, 20 © AFP

Watu watano wanazuiliwa nchini Rwanda baada ya kujaribu kutoa rushwa na kutishia mashahidi katika lengo la kufuta adhabu aliyopewa waziri wa zamani wa mipango miji wa Rwanda kuhusiana na mauaji ya kimbari nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Hukumu dhidi ya waziri huyo wa zamani wa Rwanda ilitolewa na mahakama ya Umoja wa Mataifa yenye makao yake makuu katika nchi jirani ya Tanzania, mahakama hiyo imetangaza.

Vibali vya kukamatwa dhidi ya Maximilian Turinabo, Nzabonimpa Anselme, Jean de Dieu Ndagijimana, Marie Rose Fatuma na Dick Prudence Munyeshuli vilitolewa Agosti 24, na watano hao walikamatwa nchini Rwanda Jumatatu wiki hii.

Tangu mwaka 2010, Utaratibu wa Mahakama za Kimataifa za Uhalifu za Umoja wa Mataifa Uhalifu zinashughulikia kesi zilizowekwa kiporo na ambazo ziko chini ya Mahakama ya zamani ya Kimataifa ya Uhalifu ya Rwanda (ICTR) mjini Arusha (kaskazini mwa Tanzania) iuliyowekwa ili kuwahukumu watuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo watu kutoka jamii ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo mkali 800,000 waliuawa.

Kwa mujibu wa mahakama watano hao "walitoa hongo na kkufanya vitisho kwa ushawishi mashahidi" katika kesi ya Augustin Ngirabatware, waziri wa zamani wa serikali ya Rwanda aliyehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na ambaye rufaa yake itasikilizwa mnamo mwezi Septemba.

Watuhumiwa hao watano wanatarajiwa kuhamishiwa katika mahakama ya kimataifa yenye makao yake makuu mjini Arusha, nchini Tanzania.