BURUNDI-UN-MACHAFUKO-SIASA-USALAMA

Tume ya Umoja wa Mataifa yamhusisha Rais Nkurunziza kwa machafuko Burundi

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza. REUTERS/Evrard Ngendakumana

Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Burundi imewasilisha ripoti yake mjini Geneva kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo mwaka huu na mwaka jana.

Matangazo ya kibiashara

Tume hiyo inashutumu ukiukaji mkubwa unaoendelea ambapo baadhi ya visa hivyo ni uhalifu dhidi ya ubinadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji, watu kuuawa wakiwa mikononi mwa maafisa wa serikali, watu kutoweka, visa vya watu kukamatwa kiholela na kuwekwa kizuizini kinyume cha sheria, mateso na ukatili mwingine, unyama au udhalilishaji.

Kwa mara ya kwanza, uchunguzi wa tume ya Umoja wa Mataifa unamhusisha moja kwa moja Rais Pierre Nkurunziza kwa kutoa "wito wa kuchochea chuki na uhasama".

Kutokana na ushahidi tuliokusanya, Imbonerakure, vijana wa chama tawala CNDD-FDD, wanahusika pakubwa katika visa hivyo, amesema Doudou Diène, mwenyekiti wa tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa ambaye amebaini kwamba Rais Pierre Nkurunziza "anahusika moja kwa moja katika kuchochea chuki na machafuko".

Hata hivyo ofisi ya rais wa Burundi imekanusha madai hayo na kusem akwamba ni shutma zilizotengenezwa na baadhi ya nchi za Magharibi.

Doudou Diene amepuuzia mbali kuwa hotuba ya Rais Pierre Nkurunziza imekua ikizingatia masuala ya kuboresha maridhiano, mshikamano wa kijamii.

Kwa kweli tumezoea na aina hizo za uongo, amesema Jean-Claude Karerwa, msemaji wa Rais Nkurunziza.