Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-JESHI-KIIR

Wanajeshi 10 wa Sudan Kusini wapatikana na kosa la ubakaji na wizi

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Mahakama ya Kijeshi nchini Sudan Kusini, imewakuta na hatia wanajeshi 10 kwa kuwabaka wafanyikazi watano kutoka nchi hiyo waliokuwa wanatoa misaada ya kibinadamu.

Matangazo ya kibiashara

Imebainika kuwa, wanajeshi hao walivamia Hoteli walimokuwa wafanyikazi hao na kumuua mwanahabari aliyekuwa nao John Gatluak.

Jaji wa Mahakama hiyo Knight Baryano Almas, wanajeshi hao wanahusika na makosa ya ubakaji, mauaji, wizi na uharibifu.

Kati ya wanajeshi hao 10, wawili wamepewa kifungo cha maisha huku wengine wakifungwa jela kati ya miaka 7 na 14.

Mahakama hiyo imeitaka serikali ya Sudan Kusini imewalipe fidi Dola 4,000 kwa wale wote waliobakwa na Dola zingine Milioni 2 kwa mali za hoteli hiyo zilizoharibiwa.

Hata hivyo, familia ya Gatluak, mwanahabari aliyeuliwa itapewa ngo'ombe 51.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.