TANZANIA-SIASA-USALAMA

Tundu Lissu: Nitarudi Tanzania kuendelea na shughuli za siasa

Mwanasiasa mashuhuri wa upinzani Tanzania, Tundu Lissu akizungumza katika Hospitali ya Nairobi Januari, 2018
Mwanasiasa mashuhuri wa upinzani Tanzania, Tundu Lissu akizungumza katika Hospitali ya Nairobi Januari, 2018 The Citizen

Mwanasiasa mashuhuri wa upinzani nchini Tanzania, Tundu Lissu amesema mwaka mmoja tangu aliposhambuliwa kwa risasi umekuwa mrefu na mgumu, akieleza licha ya matatizo yote amelikumbuka bunge la Tanzania na kueleza atarejea nchini humo kuendelea na shughuli za kisiasa.

Matangazo ya kibiashara

Mchana wa Septemba 7, 2017 Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa Mkoani Dodoma, punde baada ya kuhudhuria vikao vya bunge la Tanzania.

Katika waraka aliotuma kwa vyombo vya habari, Lissu amegusia mambo mbalimbali yaliyotokea tangu kushmbuliwa kwake ikiwemo suala la bunge kutogharamia matibabu yake naa kutokamatwa kwa watu waliohusika na shambulio dhidi yake.

”Hadi ninapoandika haya, hakuna mtu yeyote anayeshukiwa kunishambulia. Hakuna yeyote anayetuhumiwa.hakuna yeyote aliyehojiwa na wapelelezi wa polisi kama shahidi,’amesema mwanasiasa huyo ambay

Wakati anashambuliwa Lissu, mbali na kuwa Mbunge wa Jimbo la uchaguzi la Singida Mashariki lililopo Mkoani Singida alikuwa Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (Tanganyika Law Society) na Mwanasheria Mkuu wa Chama Kikuu cha Upinzani cha Chadema.

Kuhusu, bunge la Tanzania kutogharamia matibabu yake, Lissu ambaye amefanyika upasuaji mara 21 amesema familia yake italipeleka suala hilo mahakamani ili mahakama itoe tafsri sahihi ya jambo hilo.

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai alitoa tamko rasmi kuwa bunge la Tanzania halitagharamia matibabu ya mbunge huyo kwa madai ya kutofuata utaratibu wa wagonjwa wanaotakiwa kwenda nje kwa matibabu.

Akizungumzia hatima yake kisiasa, Lissu amesema madaktari watakapomwambia amepona atarudi Tanzania kuendelea na siasa.

“Nimewamiss watanzania, nimewamiss wananchi wa Singida Mashariki. Nitarudi Tanzania kuendela na siasa, moyo wangu hauna wasiwasi wowote licha ya shambulio hili,”ameeleza.

Kabla ya kushambuliwa kwa risasi, Lissu alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Rais John Magufuli na mara kadhaa alijikuta akikamatwa na vyombo vya dola.

Sikiliza mahojiano baina ya Tundu Lissu na mwandishi wetu Fredrick Nwaka