KENYA-MAREKANI-UGAIDI

Marekani yamtaja raia wa Kenya anayefadhili Islamic State

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump MANDEL NGAN / AFP

Wizara ya fedha nchini Marekani imemwekea vikwazo na kumtangaza mtu hatari raia wa Kenya Waleed Ahmed Zein, kama mmoja wa watu anayefadhili kifedha kundi la kigaidi la Islamic State.

Matangazo ya kibiashara

Zein, alikamatwa jijini Naiorbi mwezi Julai baada ya uchunguzi kubaini kuwa amekuwa akitoa ufadhili huo na kwa mujibu wa sheria za Marekani, yeye ni gaidi.

Marekani inasema kati ya mwaka 2017 na 2018 alituma Dola 150, 000 kusaidia shughuli za kundi hilo nchini Syria, Libya na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kenya imekuwa mshirika wa karibu wa Marekani katika vita dhidi ya ugaidi tangu mwaka 1998, wakati Ubalozi wa Marekani uliposhambuliwa jijini Nairobi.

Hivi karibuni, rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alizuru Marekani na kukutana na rais Donald Trump ambaye aliahidi kuendeleza ushirikiano wa karibu wa kupambana na ugaidi na taifa hilo la Afrika Mashariki.

Marekani pia imekuwa katika mstari wa mbele, kuungana na Kenya kupambana na kundi la kigaidi la Al Shabab nchini Somalia.