UGANDA-MUSEVENI-SIASA

Rais Museveni kulihotubia taifa Jumapili

Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Rais wa Uganda Yoweri Museveni REUTERS/Tiksa Negeri/File Photo

Rais wa Uganda Yoweri Museveni anatarajiwa kulihotubia taifa siku ya Jumapili jioni, kueleza masuala mbalimbali yanayolikabili taifa hilo la Afrika Mashariki. 

Matangazo ya kibiashara

Itakuwa ni hotuba yake ya kwanza, tangu kuzuka kwa machafuko ya kisiasa Kaskazini mwa nchi hiyo mwezi uliopita na hata msafara wake kudaiwa kurushiwa mawe.

Rais Museveni, anatarajiwa kufafanua madai ya serikali kuwapiga na kuwatesa wabunge wa upinzani na wafuasi wao wakiongozwa na Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine ambaye anapata matibabu nchini Marekani.

Kupitia machapisho mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii, serikali ya Uganda imekuwa ikikanusha madai ya kuteswa kwa wanasiasa wa upinzani lakini inakiri kuwa walipigwa.

Wiki hii akizungumza kwa mara ya kwanza akiwa Marekani, Bobi Wine aliielezea namna alivyoumizwa na wanajeshi na kuapa kuwa ni lazima atarejea nyumbani baada ya kupata matibabu.