TANZANIA-AJALI

Watu 15 wapoteza maisha katika ajali ya barabarani nchini Tanzania

Ajali ya barabarani mjini Mbeya Septemba 07 2018
Ajali ya barabarani mjini Mbeya Septemba 07 2018 MwananchiNews

Watu 15 wamepoteza maisha na wengine 13 kujeruhiwa baada ya Lori lililokuwa linasafirisha viazi Kusini mwa Tanzania, kugonga magari matano.

Matangazo ya kibiashara

Polisi katika eneo hilo wanasema, lori hilo lilipoteza mwelekeo katika mteremko mkali, Ijumaa usiku.

“Tumeshuhudia ajali nyingine, ambayo imesabisha wananchi wenzetu kupoteza maisha. Nimesikitishwa sana na maafa haya,” amesema rais wa nchi hiyo John Magufuli.

Ajali hiyo imehusisha malori matrela mawili yanayosafirisha mafuta ya petroli, malori mawili na mabasi mawili madogo ya abiria.

Ajali za barabarani nchini Tanzania zimekuwa zikishuhudiwa mara kwa mara, sababu kubwa ikiwa ni  tabia ya madereva kuendesha magari kwa mwendo wa kasi.

Ubovu wa magari na maafisa wa polisi wa barabarani kutosimamia ipasavyo utekelezwa wa sheria za barabarani zimeelezwa kuwa sababu ya ongezeko la ajali nchini humo.