TANZANIA-UFARANSA-BIASHARA

Maseneta kutoka Ufaransa wafanya ziara nchini Tanzania

Kutoka kushoto ni Benard Jomier,Balozi Frederic Clavier, Ronan Dantec,na Cyril Pellevant wakizungumza na waandishi wa Habari
Kutoka kushoto ni Benard Jomier,Balozi Frederic Clavier, Ronan Dantec,na Cyril Pellevant wakizungumza na waandishi wa Habari Ericky Boniphace/Dar es salaam

Manaseneta kutoka nchini Ufaransa wamekutana na viongozi mbalimbali wa serikali ya Tanzania na kujadili namna ya kushirikiana katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na namna ya kuongeza idadi ya watalii nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumzia umuhimu wa ziara hiyo ya juma moja,Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier amesema ushirikiano kati ya Tanzania na Ufaransa unalenga kuboresha sekta mbalimbali nchini humo licha ya kuongeza ufadhili mara mbili zaidi katika miradi ya maendeleo kutoka Euro Milioni 50 na kufikia euro milioni 100.

Kiongozi wa Maseneta hao Ronan Dantec, akizungumza kwa niaba ya Maseneta Cyril Pellevant, Benard Jomier amesema wamedhamiria kushirikiana na serikali ya Tanzania katika nyanja mbalimbali ili kufikia adhima ya maendeleo hasa kwenye Utalii .

Seneta Dantec amesema hatua hiyo imewasukuma kujadili namna ya kushirikiana katika sekta za Nishati, Mazingira na Utalii.

“Sababu ya pili kubwa ya ziara yetu ni kuongeza uhusiano na kuangazia urithi wa kipekee uliopo Tanzania na Utalii,utalii pya kwa sababu utalii unaendelea kukua ipo tofauti na miaka 30 iliyopita” alisema Dantec.

Katika ziara hii tayari Maseneta hao wamekutana na Mawaziri wa Tanzania katika wizara za Nishati,Maji na Umwagiliaji,Mali asili na Utalii pamoja na Waziri wa nchi anayeshughulikia Muungano na Mazingira na watahitimisha kwa kuelekea visiwani Zanzibar.