KENYA-UCHUMI

Rais Kenyatta akubali kupunguza kodi ya mafuta hadi asilimia 8

Iwapo Kenya itazidi kushukishwa uwezo wake wa kukopesha, hilo linaweza kuchangia kwa nchi hiyo kuishia kuchukua mikopo kwa viwango vikubwa vya riba.
Iwapo Kenya itazidi kushukishwa uwezo wake wa kukopesha, hilo linaweza kuchangia kwa nchi hiyo kuishia kuchukua mikopo kwa viwango vikubwa vya riba. RFI-KISWAHILI

Rais Kenyatta amewaonea huruma raia wake na kukubali kupunguza bei ya bidhaa ya mafuta kutoka 16% hadi 8%. Katika hotuba kwa taifa, Rais Uhuru Kenyata amesema kuwa amesikia kilio cha Wakenya kuhusu kupanda kwa bei za bidhaa mahitajio na usafiri.

Matangazo ya kibiashara

Mbali na kupunguza kodi ya mafuta, Rais Kenyatta amepinguza gharama za mapokezi , burudani, mafunzo na mikutano, na usafiri katika nchi za nje.

Hata hivyo amependekeza kuongezwa fedha katika idara za utekelezaji wa sheria na hivyo kuweza kukusanya kipato zaidi kupitia mahakama nchini.

Mapendekezo yote hayo ya Rais Kenyatta yanasubiri kuidhinishwa bungeni wakati wa kikao maalum Septemba 18.

Hata hivyo bado serikali ya Kenya ina kazi kubwa ya kulishawishi Shirika la Fedha Dunia IMF na kujua wapi itakapopata zaidi ya dola milioni 90 kuziba pengo katika nakisi ya bajeti.

Kenya inakabiliwa na ongezeko la deni la taifa ambalo kwa sasa linakadiriwa kuwa limefika 58% ya pato jumla la nchi, kwa mujibu wa shirika la kimataifa la kuorodhesha uwezo wa mataifa kukopa, Moody.

Kwa sasa wananchi wa Kenya wamejawa na furaha, huku kila kona ukiwakuta watu wakizungumzia uamuzi huu wa rais Uhuru Kenyatta.