UGANDA-SIASA-USALAMA-HAKI

Bobi Wine aamua kurudi kampala, polisi yaonya

Mwanamuziki na mwanasiasa Bobi Wine wakati wa maandamano huko Kampala Julai 11, 2018.
Mwanamuziki na mwanasiasa Bobi Wine wakati wa maandamano huko Kampala Julai 11, 2018. Isaac Kasamani / AFP

Mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi anayefahamika kwa jina la Bobi Wine, anarejea nyumbani hivi leo akitokea nchini Marekani alikokuwa anapata matibabu.

Matangazo ya kibiashara

Polisi wametoa onyo kuwa hakuna atakayeruhusiwa kuandamana au kwenda kumpokea mwanasiasa huyo katika uwanja wa ndege, isipokuwa familia yake ya karibu.

Hata hivyo, huenda kukashuhudiwa kwa makabiliano kati ya polisi na wafuasi wa mwanasiasa huyu ambaye ana ushawishi mkubwa hasa miongoni mwa vijana.

Alitarajiwa kurudi nyumbani Jumatatu wiki hii, lakini hakutoa sababu za kuahirishwa safari yake.

Juma moja lililopita amlisema licha ya hofu ya kukamatwa na kufanyiwa madhila mengine ameamua kurudi nyumbani kutetea wanyonge.

Mwanasiasa huyo ambaye pia ni mwanamuziki maarufu nchini Uganda kwa sasa yupo Marekani anapopatiwa matibabu baada ya kupigwa na maafisa wa usalama wa Uganda.